Simba ili kutumia Uwanja wa Amaan ilipie Mil 200

Licha ya Kamishna wa Michezo Zanzibar, Ameir Mohammed Makame mapema jana kufafanua kuwa, imewaita Simba mezani ili kujadiliana nao kwa lengo la kulipa Dola 75,000 (sawa na Sh 200 Milioni) ili kupeleke mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwenye Uwanja wa New Amaan, taarifa nzuri kwa mashabiki wa Msimbazi ni kwanza CAF imebariki mechi kupigwa visiwani humo.
.
Simba itaikaribisha Stellenbosch ya Afrika Kusini katika mchezo wa awali utakaopigwa Jumapili hii kabla ya kuifuata Sauzi wiki moja baadae, huku uwanja iliyoutumia kuing’oa Al Masry ya Misri katika hatua ya robo fainali, Benjamin Mkapa kufungiwa kwa muda ili ukarabatiwe.
.
Mapema jana asubuhi, Kamishna wa Michezo Zanzibar, Ameir Makame, ambaye alisema ilikuwa haijawa rasmi juu ya mchezo huo kuhamishiwa Zanzibar, lakini baadae mchana chanzo makini hili lilidokezwa CAF imeshatuma barua pepe kubariki kupigwa visiwani humo.
.
“Ni kweli Simba wameomba kutumia Uwanja wa Amaan, lakini makubaliano bado hayajafikia mwisho kwani wizara imeitaka Simba kulipia gharama ambazo kiuhalisia ni kubwa sana Dola 75,000 (karibu Sh 200 milioni). Gharama hiyo, Simba imesema ni kubwa sana na kuahidi kufanya mazungumzo na Wizara.” alisema Ameir.
.
Hata hivyo, taarifa kutoka ndani ya Simba zinasema tayari kila kitu kimekaa sawa.
cc;Sportarena X account