Michezo

Simba kukipiga leo hii KMC Stadium

Baada ya Kushindwa kuchezwa kwa Mechi ya Dabi ya Kariakoo, leo jioni Simba inatarajiwa kushuka Uwanjani kuvaana na TMA Stars ya Arusha ukiwa ni Mchezo wa hatua ya 32 bora wa Michuano ya Kombe la Shirikisho (FA)


.
Hii ni kati ya mechi tatu za Michuano hiyo zinazopigwa leo, Ukiwemo ule wa Kiluvya dhidi ya Pamba Jiji, na Kagera Sugar itakayokuwa wenyeji wa Namungo, huku Simba ikiwa mwenyeji dhidi ya Maafande wa TMA iliyopo Ligi ya Championship (daraja la Kwanza).


.
TMA inayofundishwa na Kocha Mohamed Ismail ‘Laizer’ ipo nafasi ya tano katika Ligi daraja la Kwanza, itashuka uwanjani kukabiliana na Simba iliyopo nafasi ya pili katika Ligi Kuu na hatua ya Robo fainali ya Kombe la Shirikisho CAF na ikiwa na kikosi chenye wachezaji wenye uchu wa kufumania nyavu, Leonel Ateba, Jean Ahoua na Steve Dese Mukwala.


.
Kwa mujibu wa Kanuni 😀 za mechi za raundi hizo za awali, timu zikitoka sare ndani ya dakika 90 Mshindi atapatikana kupitia mikwaju ya penati.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents