Michezo

Simba kumchukua pacha wa Aziz Ki

Imeripotiwa kwamba, Klabu ya Simba ipo kwenye mazungumzo na beki wa kushoto wa timu ya taifa ya Burkina Faso  na FC Lupopo ya DR Congo, Valentin Nouma (24) kwa ajili ya kuipata huduma yake. 

Simba ambayo imepanga kujiimarisha zaidi kuelekea msimu ujao, inaamini kwamba beki huyo anayecheza kikosi cha Burkina Faso sambamba na kiungo wa Yanga Stephane Aziz Ki, anaweza kuwa mtu sahihi kwao.

Uamuzi wa Simba kusaka beki wa kushoto umekuja baada ya kumtumia kwa muda mrefu nahodha wao, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ ambaye anaonekana mpinzani wake ameshindwa kupatikana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents