Michezo

Simba Queens watinga Bungeni, Naibu Waziri Gekul awapongeza kwa Ubingwa

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul ameipongesa timu ya wanawake ya Simba Queens kwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya wanawake (Serengeti Lite Women Premier League)

“Nina wapongeza viongozi, benchi la ufundi pamoja na wachezaji wote kwa juhudi kubwa mlizo onesha katika kipindi chote cha ligi na kuweza kuwa mabingwa kwa mara ya pili mfululizo” Gekul.

“Ligi ilikuwa na ushindani mkubwa lakini mmeweza kuibuka washindi, hii ni ishara kuwa ligi yetu ya wanawake inazidi kuimarika” – Gekul

Timu ya Simba Queens imepata mwaliko maalumu wa kutembelea bungeni leo tarehe 17 Mei, 2021 mara baada ya kutwaa taji la ligi ya wanawake kwa kuifunga timu ya Baobab Queens goli moja bila katika mchezo uliofanyika jana kwenye uwanja wa jamhuri jijini Dodoma.

 

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents