Simba ruksa mashabiki 10,000 – CAF

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeiruhusu timu ya Simba kuingiza washabiki 10,000 katika mechi yao dhidi ya AS Vita.

Kwa mujibu wa Shirikisho hilo la soka nchini, Simba imeruhusiwa kuingiza idadi ya mashabiki 10, 000 kutokana na maombi ya TFF.

Simba itawakabili AS Vita Club siku ya Jumamosi ya Aprili 3, 2021 katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar Es Salaam huku ikiwa na kumbukumbu ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0 Kinshasa nchini Congo.

Related Articles

Back to top button