Michezo
Simba SC waihofia Ihefu

Simba SC wamesema mchezo wao dhidi ya Ihefu FC hautakuwa rahisi kwani wamesajili wachezaji wenye uzoefu.
Kocha msaidizi Selemani Matola ametoa kauli hiyo alipokuwa akiuzungumzia mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC unaotarajiwa kupigwa Kesho April 13, 2024 katika Uwanja wa CCM Liti, Singida.
“Haitakuwa rahisi, Ihefu imesajili wachezaji wengi wazuri na wenye uwezo, ushindani utakuwa mkubwa ila naamini kwenye maandalizi yetu na tumejipanga kupata ushindi,” alisema Matola.
Imeandikwa na Mbanga B.