Michezo

Simba sio mbovu kama wanavyosema watu – Azim Dewji

“Simba sio mbovu kama ambavyo wengi wanaona, shida kubwa hapa ni ubora ambao wanao Yanga na Azam kwasasa wakati kikosi chetu kikiwa na mapungufu machache yanayotokana na ubora,”alisema Dewji.“

“Simba ili itoke hapa kwanza viongozi wetu wanatakiwa kutoka hadharani na kuongea na mashabiki wao ikibidi hata kuitisha mkutano, baada ya hapo wawaeleze mipango yao ya kuitoa timu hapa ilipofika watu wataelewa na huo mkakati ukafanye kazi kwelikweli.”

“Hakuna mwekezaji ambaye atatoa fedha za kununua wachezaji akavumilia kuona usajili unaofanyika haukidhi viwango, kama kuna changamoto za ubora wa wachezaji wakati huu viongozi wahakikishe hayo hayajirudii, pia mashabiki wanatakiwa kuelewa sio kila mchezaji akisajiliwa basi atafanya vizuri kwa haraka kama ambavyo alikuwa kule anakotoka.”

— Mfadhili wa zamani wa Simba, Azim Dewji.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents