
Mwenyekiti wa Klabu, Murtaza Mangungu amesema kuwa wameshafanya maandalizi kwaajili ya kumvaa Raja Casablanca Jumamosi ya Februari 18, 2023 Benjamin Mkapa.
”Maandalizi yote yanayotakiwa kufanyika ndani na nje ya uwanja yamefanyika, lengo letu ni kuhakikisha mashabiki wanaujaza uwanja wote wa Benjamin Mkapa.”-Mwenyekiti Murtaza Mangungu
Mangungu ameongeza ”Sio mara ya kwanza kucheza mechi kubwa kama hii, wachezaji wanajua umuhimu wa mchezo huu. Ilitokea bahati mbaya tukapoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Horoya ugenini hilo hatutaki lijirudie tena.”
Murtaza Mangungu ameyasema hayo wakati wa Uzinduzi wa kampeni ya hamasa kuelekea huo wa pili wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco.
Credit @fumo255