HabariMichezo

Simba wajipanga na shirikisho la Azam

Kikosi cha Simba SC kimerejea mchana jijini Dar es Salaam kutoka Dodoma baada ya ushindi mwembamba wa goli 1-0 waliopata dhidi ya Dodoma Jiji.

Baada ya kufika wachezaji wamepewa mapumziko na kesho kikosi kitarejea mazoezini kujiandaa na mchezo wa Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Jumamosi, Benjamin Mkapa.

Wachezaji wote wa Simba SC wanatarajiwa kushiriki kwenye mazoezi hayo yatakayofanyika Uwanja wa Mo Simba Arena baada ya kukosekana kwenye mechi ya jana kutokana na kadi tatu za njano na wengine kuwa majeruhi.

Related Articles

Back to top button