Bongo5 ExclusivesHabariMichezo

Simba wampa mkono wa kwaheri beki wao kisiki Pascal Wawa

Klabu ya Simba imeamua kuacha na beki wake wa kati raia wa Ivory Coast Pascal Wawa baada ya mkataba wake kumalizika kwenye klabu hiyo yenye makazi yake Msimbazi Kariakoo.

Kupitia Instagram yao wamemuaga mchezo huyo huku wakisema mchezo wa Simba dhidi ya Mtibwa ndio utakuwa mchezo wake wa mwisho wa kuitumikia klabu hiyo.

Wawa ameitumikia Simba kwa takribani miaka minne huku akifanikiwa kutwaa mataji mbalimbali yakiwemo Ligi kuu.

Kupitia Instagram yao wameandika kuwa: 𝗔𝗦𝗔𝗡𝗧𝗘 𝗣𝗔𝗦𝗖𝗔𝗟 𝗪𝗔𝗪𝗔 Baada ya kutumikia timu yetu kwa misimu minne, Pascal Wawa hatakuwa sehemu ya kikosi chetu cha msimu ujao. Mkataba wake utamalizika mwisho wa mwezi huu na mchezo wa Alhamisi dhidi ya Mtibwa Sugar utakuwa mchezo wake wa mwisho. #NguvuMoja

Related Articles

Back to top button