HabariMichezo

Simba wamsamehe Chama, aondoka Dar kuelekeza Kigoma

Simba tayari wamemsehe @realclatouschama baada ya kumsimamisha kwa masuala ya kinidhamu.

Klabu hiyo imeweka ujumbe inaosomeka kuwa

“Uongozi wa Klabu ya Simba unapenda kuwataarifu Wanachama na Wapenzi wa Simba kuwa umemsamehe mchezaji Clotus Chama.

Hatua hii imefuatia maamuzi ya Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Simba ambayo ilipitia barua ya maelezo ya Chama na pia amuzi wa Kocha Benchica a kumsamehe Chama, hivyo Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Simba ikaridhia kumsamehe na kusitisha kumfikisha kwenye Kamati ya maadili ya Klabu ya Simba.

Chama anaungana na Kikosi cha Simba kilicho Mkoani Kigoma kwa mchezo wa ligi kuu ya NBC.

Klabu ya Simba itaendelea kutilia mkazo ustawi wa nidhamu kama nguzo muhim ya kujenga timu imara. Nidhamu ni moja ya tunu (Values) za klabu ya Simba.

Tayari Chama yupo njiani na msemaji wa klabu hiyo @ahmedally_ wanaenda kuungana na timu Kigoma baada ya wachezaji wengine kuwasili jana kwa mchezo dhidi ya Mashujaa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents