Michezo
Simba, Yanga tofauti ni point 2, Azam FC yapotea ‘Big Four’, je ligi ngumu msimu huu ?
Msimamo wa Ligi Kuu ya NBC mpaka leo Disemba 13, 2021 baada ya Kukamilika kwa michezo ya mzunguko wa nane. Mabingwa wa Kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara Young Africans Sports Club wanaongoza kwenye msimamo wa Ligi kwa kuwa na point 20 nyuma ya Mabingwa watetezi Simba wenye alama 18 tofauti ya point mbilitu huku Matajiri wa Jiji la Dar Es Salaam Wanalambalamba Azam FC wakipotea kabisa kwenye nafasi nne za juu wakiwa kwenye nafasi ya saba (7) na alama zao 11 tofauti na matarajio ya wapenzi wengi wa soka hasa kutokana na usajili mkubwa waliyofanya katika kipindi cha dirisha la usajili lililopita.
Imeandikwa na @fumo255