Michezo
Simba yaoga minoti ya kutosha

Kitendo cha Simba kutinga Nusu fainali kimeifanya timu hiyo kujihakikishia kiasi cha dola 750,000 (zaidi ya Sh 1.9 bilioni) kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kama zawadi ya kutinga hatua hiyo.
Lakini si hivyo tu, nyota wa timu hiyo wamelamba fedha nyingine kutoka kwa mabosi wao wakiongozwa na bilionea na mfanyabiashara maarufu Mohamed Dewji ‘Mo’ kama sehemu motisha ambapo ni Sh 500 milioni.
Huku kwa upande wa wachezaji waliotoa pasi za mabao (asisti) ambao ni Kapombe na Tshabalala pamoja na waliotikisa nyavu, Mpanzu na Mukwala watalamba Sh3 milioni kila mmoja.
Pia wachezaji wa Simba wamevuna mkwanja mwingine kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan @SuluhuSamia ambaye alitangaza kutoa Sh10 milioni kwa kila bao litakalofungwa hivyo katika mabao mawili Simba imepata Sh20 milioni.