Sina mpango wa kuondoka SharoBaro – HitBits

Hayo yamebainishwa na mtayarishaji wa muziki kutokea studio za sharobaro, Hit Bits alipokuwa akiongea na Bongo5 kufuatia stori inayozunguka kuhusu kufungua studio yake maeneo ya kimara.

Mtayarishaji huyo amesema, uwepo wake hapo unampatia nafasi ya kufanya kazi zake kwa uhuru tofauti na studio zingine.

“Bado nipo sana, sharobaro na sina mpango wakuondoka na nitaendelea kutengeneza ngoma kali. Kwa sasa studio yetu ina project kali zinakuja kutoka kwa Bob mwenyewe na wasanii wengine kama Baraka da prince na chipukizi” amesema Hit Bits.

Hits ni maarufu kuatayarisha nyimbo kama vile chuku chuku ya Bob Junior,Nyamiela ya Nasiri na zingine za wasanii wachanga.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button