Michezo

Singida Big Stars yauzwa na kupewa jina jipya

Klabu ya Singida Big Stars imeuzwa kwa Fountain Gate na rasmi leo Juni 14, 2023 timu hiyo itatambulika kama Singida Fountain Gate FC.

Akizungumza na waandishi wa habari Rais wa timu hiyo, Japhet Makau amesema kuwa wameichukua kwa asilimia 100.

“Tumechukua 100% ya umiliki wa Singida Big Stars,”- Rais wa Singida Fountain Gate FC Japhet Makau

Makao ameongeza kuwa Singida Fountain Gate FC haitafungamana na timu nyingine “Singida Fountain Gate FC haifungamani na timu yoyote.”

Olebile Sikwane kutoka Botswana ametambulishwa kuwa Mtendaji Mkuu wa Singida Fountain Gate FC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents