Habari

Siogopi kumvua mtu madaraka, siwaachi salama – Naibu waziri Silinde (+Video)

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Mkoa wa Mwanza Mpandalume Simon Mpandalume ameuomba uongozi wa Wilaya ya Magu kupitia Mkuu wa Wilaya kumuita na kumuhoji mkuu wa shule ya sekondari ya Kabila Edgar Karokora  kwa matumizi mabaya ya fedha na usimamizi mbovu wa fedha za serikali zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa bweni katika shule hiyo.

Hayo yamejitokeza baada ya ziara ya Naibu Waziri wa Tamisemi David Silinde kufika katika shule hiyo nakukuta ujenzi bado unasusua huku fedha zote za mradi milioni 80 zikiwa zimekwisha bila jengo kukamilika na muda wa ujenzi ukiwa umeisha siku zake.

Mwenyekiti Mpandalume  amesema kuna haja ya kuwaita wote wanaohusika na usimamizi wa jengo hilo kuhojiwa na kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu ma kisheria kwa kuharibu fedha za siku huku wao kama halmshauri kutumia fedha za mapato ya ndani kukamilisha ujenzi huo kwa wakati.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa TAMISEMI David Silinde ametaka ujenzi wa bweni hilo ukamilike ndani ya mwezi mmoja na nusu na ifikapo mei ata kwenda kukagua jengo hilo huku akiagiza mkuu wa shule,afisa elimu wa wilaya na mhandisi kuandika barua ofisi ya Rais Tamisemi kwanini ujenzi huo umechelewa kukamilika na wakishindwa kukamilisha atawavua madaraka yao.

Katika hatua ya kujitetea Mkuu waa shule ya sekondari ya Kabila Edgar Karokora amesema kikichochelewesha ujenzi kukamilika kwa wakati ni upatikanaji wa shida wa saruji na mabati wakati wa kuanza kutekeleza mradi na umbali wa upatikanaji wa mali ghafi hali iliyopelekea gharama za ujenzi kua kubwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents