Michezo

Siondoki AS Roma –  Jose Mourinho baada ya kuhusishwa na Everton

Jose Mourinho baada ya kuhusishwa kurejea England kuifundisha Everton, mwenyewe afunguka na kusema kuwa kamwe hana mpango wa kuachana na AS Roma mpaka pale atakapo maliza kandarasi yake ya miaka mitatu.

‘’Nimesema kwamba kwa sasa ninayo furaha na kamwe siwezi kuvunja ‘project’ yangu na AS Roma. Niliwaahidi kwa hii miaka mitatu na siwezi kuondoka kabla ya miaka mitatu kwisha, huu ni mradi wangu pia.”

Everton ipo katika harakati za kutafuta kocha mpya atakayeweza kurithi mikoba ya Rafa Benitez aliyetimuliwa kazi Jumapili iliyopita, katika wakati huu ambapon nafasi yake ya muda ikichukuliwa na Duncan Ferguson.

Ukiachia mbali Mourinho, wengine wanaodaiwa kuwa kwenye listi ya kuifundisha Everton ni pamoja na Roberto Martinez, Wayne Rooney na Frank Lampard kwa mujibu wa Sky Sports.

Kwa sasa AS Roma ipo kwenye nafasi ya saba (7) wa msimamo wa ligi ya Serie A, wakiwa na alama 35 huku kinara wakiwa Inter wenye point 50.

 

Related Articles

Back to top button