Smashed yazinduliwa kudhibiti unywaji wa Pombe kwa Vijana WenyeUmri Mdogo
Kampuni ya Bia ya Serengeti Limited (SBL) inapenda kutangaza muendelezo waProgramu ya Smashed katika Mkoa wa Tanga. Programu hii inatoa ya elimu kupitia maonyesho kwakulenga kuvunja utamaduni wa kunywa pombe kwa vijana wenye umri mdogo na kupunguza madharayanayohusiana na pombe kwa vijana. Programu yaSmashed ya Kampuni ya Bia ya Serengeti inawakilishahatua muhimu kuelekea kukuza uchaguzi wenyedhamira na kuwawezesha vijana wa Tanzania kuwa namaarifa na stadi wanazohitaji kufanya maamuzi sahihikuhusu matumizi ya pombe na kuzuia kabisa matumiziya pombe kwa vijana walio chini ya umri wa kisheria.
Utafiti uliofanywa na Wizara ya Afya na Ustawi waJamii mwaka 2008 miongoni mwa wanafunzi wa shuleza sekondari katika Mkoa wa Dar es Salaam uligunduakuwa asilimia 5 walitumia pombe, asilimia 10.8 walishatumia pombe kabla ya kufikisha miaka 14, naasilimia 26.2 walikuwa na mzazi aliyekuwa anatumiapombe. Matumizi ya pombe wakati wa utoto na ujanayanaweza kuwa na athari mbaya za kiafya, kijamii, kiuchumi, na kimaendeleo kwa vijana na jamii. Utafitiunaonyesha kuwa vijana wanaoanza kunywa pombe kabla ya umri wa miaka 15 wako mara sita zaidi kwa hatari ya kuwa na matatizo ya utegemezi wa pombe kuliko wale wanaoanza kunywa baada ya umri wamiaka 21.
Kutokana na hili, Kampuni ya Bia ya Serengeti Limited illianzisha programu hii mwaka 2021, na tayariimekuwa na mchango mkubwa kwa vijana wetu. Hadileo, SBL imefikia shule 22, ikiwaelimisha zaidi yawanafunzi 24,025 kote nchini. Programu hii haihusishitu uzuiaji wa kutumia pombe kwa vijana, bali pia kuwezesha akili za vijana wetu kufanya maamuzi yenyemsingi na dhamira sahihi. Inawatia moyo wanafunzikutilia maanani elimu yao na kuendeleza stadi muhimu, kama vile kutawala hisia zao, ambayo itakuwa zanamuhimu katika kushughulikia changamoto za maisha.
Rispa Hatibu, Meneja wa Mawasiliano na Uendelevuwa Kampuni ya Bia ya Serengeti Limited alisema, “SBL inaelewa kuwa shinikizo la rika haswa vijana nisababu ya kunywa pombe kwa vijana na ni muhimukukumbuka kuwa una uwezo wa kusema hapana nakufanya maamuzi yanayolingana na thamani yamalengo yako. Marafiki wa kweli wataheshimumaamuzi yako na kusaidia safari yako. Kama wanafunzi, nyote ni sehemu ya jamii kubwa zaidi nje yashule hizi, na sote tunashiriki jukumu la kujali ustawiwa wenzetu na jamii kwa ujumla. Watie moyo marafikina wenzako kufanya maamuzi sahihi na kupingakunywa pombe kwa vijana walio chini ya umri wakisheria.”