
Onyesho kubwa la mitindo lenye hadhi ya juu, Tanzania Fashion Festival linatarajiwa kurudi tena baada ya kusubiriwa kwa mwaka mzima na wapenzi wa mitindo nchini. Katika tangazo ambalo limetolewa hivi karibuni , linaonyesha tamasha la mitindo la mwaka huu litaongozwa na Smirnoff kama Mdhamini mkuu.
Ikisabambazwa na Serengeti Breweries Limited (SBL), hii ni mara ya pili mfululizo, na mara ya tatu kwa SBL kushirikiana na jukwaa hili la mitindo. Hivi karibuni, Smirnoff imeongeza aina ya vinywaji vyake, baada ya kutambulisha Smirnoff Guarana pamoja na Smirnoff Pineapple, pembeni ya Smirnoff Ice Black ambayo tayari inafahamika sana.
Tanzania Fashion Festival ni tukio la mitindo na staili za maisha, ambalo linaleta pamoja maonyesho ya mavazi yanayotengenezwa Tanzania, Muziki wa Tanzania, Jazz pamoja na dansi. Tamasha hili lilianza mwaka 2018 na mtangazaji Mashuhuri wa mitindo kwenye Televisheni na baadaye Mfanyabiashara wa masuala ya mitindo Deogratius Kithama tangaia mwaka 2018.. “Moja ya vitu ambavyo watu wanategemea siku zote kutoka kwetu ni hadhi ya juu ya mitindo na matukio ya staili za maisha kutoka kwetu. Sisi tunakuletea mitindo bora, muziki bora na dansi bora, na kila mwaka tunafanya kazi kubwa katika kuletea burudani ambazo hautozisahau’ anasema Kithama.
Katika tukio la mwaka jana, mamia ya watu walifika kwenye tukio hili la majira ya joto, huku wakimwona Miss World Africa aliyepita Nancy Sumary akifungua tamasha, onyesho kabambe kutoka kwa Mwanamuziki mashuhuri Ben Pol, na Zaidi ya wabunifu 30 wakionyesha mavazi maridadi ya Kitanzania.
Wakati , tarehe ya tukio la mwaka huu bado haijatajwa, mashabiki wanaombwa kukaa tayari kwaajili ya tukio la Tanzania Fashion Festival 2024, ambalo litakuwa ni tamasha la 7 tangia kuanzishwa kwake.
#TzFashionFestival2024 @tanzaniafashionfestival @smirnofftz