Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohammed almaarufu Farmajo, ametangaza leo kumuachisha kazi Waziri Mkuu Mohamed Hussein Roble siku moja baada ya wawili hao kuzozana kuhusu uchaguzi uliocheleweshwa kwa muda mrefu nchini humo.

Taarifa kutoka kwa ofisi ya rais imesema kuwa rais huyo aliamua kumuachisha kazi Roble na kusitisha madaraka yake kwasababu ya kuhusishwa kwake na ufisadi na pia kumshtumu kwa kuingilia uchunguzi kuhusu kesi ya unyakuzi wa ardhi.
Roble, ambaye bado hajajibu tangazo hilo la kumuachisha kazi amesema kuwa Farmajo hataki kuandaa uchaguzi wa kuaminika nchini humo.
Kwa upande wake, Farmajo amemshtumu Roble kwa kujaribu kushawishi uchunguzi wa kashfa iliyohusisha ardhi inayomilikiwa na jeshi baada ya waziri huyo mkuu kumfukuza kazi waziri wa ulinzi hapo jana na kumteua mrithi wake.