Siasa

Somalia: Wagombea 39 wajitokeza kuwania urais 

Somalia imeweka rekodi ya wagombea 39 kwa ajili ya uchaguzi wa rais tarehe 15 Mei, kamati ya bunge iliyopewa jukumu la kuunda uchaguzi huo uliocheleweshwa kwa muda mrefu imesema Jumanne.

Wabunge na maseneta watamchagua rais mpya ndani ya jengo la uwanja wa ndege wa Mogadishu wenye ulinzi mkali katika nchi hiyo ambayo inapambana na uasi wa mwongo mmoja wa wanamgambo wa kiislamu.

Miongoni mwa wagombea kuna marais wawili wa zamani, Hassan Sheikh Mohamud aliyeongoza kati ya 2012 na 2017, Sharif Sheikh Ahmed, aliyeongoza kati ya 2009 na 2012, vile vile waziri mkuu wa zamani, Hassan Ali Khaire aliyehudumu kwenye uadhifa huo kati ya 2017 na 2020.

Rais wa jimbo la Puntland Said Abdullahi Dani na waziri wa zamani wa mambo ya nje ambaye alihudumu kama waziri mdogo, Fawzia Yusuf kati ya 2012 na 2014 ni miongoni mwa waliojiandikisha kugombea.

Mgombea mshindi lazima aungwe mkono na theluthi mbili ya wabunge na maseneta, ikimaanisha angalu kura 184.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents