Siasa

Spika Ndugai: Chama kina mfumo dume iweje wabunge 19 wafukuzwe wote wanawake (+ Video)

Spika wa Bunge Job Ndugai leo amesimama bungeni kutoa ufafanuzi wa mambo kadhaa ikiwemo uwepo bungeni wa Wabunge 19 wa Viti Maalum kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo pamoja na kauli alizozitoa Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye kuhusiana na uwepo wa Wabunge hao Bungeni

Spika Ndugai amesema pamekuwa na maneno mengi ya kumshambulia kwenye mitandao ingawa yeye hapendi kushughulika na mambo ya mitandao. Ameeleza kuwa wengi wamekuwa wakilisifu Bunge la Tisa lililokuwa chini ya Spika Sitta lakini hawafahamu yeye alikuwa msaidizi wa karibu wa Spika Sitta akihudumu kama Mwenyekiti wa Bunge na ameshiriki kwa kiasi kikubwa katika kutengeneza kanuni za Bunge zinazotumika sasa.

“Mdogo wangu Nape yalimtoka maneno kidogo na yamesambaa sana huko mitandaoni, ikifika mahali Spika na Mbunge mnapishana si jambo jema, yeye ana uhuru wa kusema lakini hana uhuru wa kuwasema wabunge wenzake, nilizungumza nae na ninawaomba mumsamehe, aliwakosea sana na ninaomba sana tuchunge midomo yetu.” Alieleza Spika Ndugai

Spika Ndugai amemaliza kwa kuwataka Wabunge 19 wa Viti Maalum CHADEMA waendelee kuchapa kazi huku akisisitiza kwamba ana uzoefu wa kutosha na wanaosema amevunja katiba, hawajui wasemalo kwani yeye hawezi kufanya maamuzi kwa kuandikiwa kipeperushi bali ametaka Katibu wa CHADEMA aandike barua ikiambatanishwa na Katiba ya chama pamoja na muhtasari wa kikao kilichofanya maamuzi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents