Siasa

Spika Ndugai: Vijana wengi Tanzania si waaminifu, Ipo haja ya viongozi wa dini kuhubiri (+ Video)

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai amesema suala la uaminifu linahitaji kujadiliwa kutokana na vijana watanzania kulalamikiwa kutokuwa waaminifu kwenye miradi mbalimbali.

“tunalo tatizo katika nchi yetu la ujumla wake la uaminifu, sasa sijui hili tutalifanyaje wawekezaji wengi wamekuwa wakilalamikia uaminifu hasa wa vijana Watanzania, ikishawekwa mradi basi vijana uaminifu unakua mdogo.”
“Atajikuta mtu amefilisika tu asipoangalia yaani eneo hili sijui dawa yake ni nini lakini basi waheshimiwa wabunge watakapokua wanachangia ni moja ya eneo la kulitazama kiwango cha uaminifu ni kikubwa kwa kiasi gani.”

“Iko haja ya Viongozi wetu wa dini wa madhehebu mbalimbali kuweza kuhubiri kuhusiana na uaminifu, shuleni mitaala, na wazazi tujenge jamii ambayo ni ya watu waaminifu wasio kuwa na tamaa, leo ukiwekeza afu uje bungeni umewaachia miezi sita ujawatemebelea utakuta umepigwa” amesema Ndugai.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents