BurudaniHabari

Stamina msanii bora wa Hip Hop ukanda wa Afrika Mashariki

Msanii wa Bongo Fleva, @staminashorwebwenziameibuka kidedea baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa Tuzo ya PSMA katika kipengele cha Msanii Bora wa Hip Hop/Rap katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Tuzo hizo zimetolewa usiku wa kuamkia juzi Jumamosi katika Jiji la Bujumbura, Burundi na kuwashirikisha wasanii kutoka nchi mbalimbali za Afrika Mashariki.

Kupitia Instagram yake Stamina ameandika kuwa.

Usiku wa juzi jumamosi nilitakiwa niwe burundi katika usiku wa utoaji tuzo za @platformshow257 sema ratiba zikaingiliana na fiesta ya mwanza!!

Napenda kutoa shukrani za dhati kwa mashabiki zangu wote walionipigia kura na wadau waliosupport bila kuwasahau waandaaji wenyewe @platformshow257

Ushindi umerudi nyumbani TANZANIA…na sasa ni MSANII BORA WA RAP/HIP HOP WA AFRIKA MASHARIKI katika TUZO ZA @platformshow257 za nchini BURUNDI

JIWE WALILOLIKATAA WAASHI LIMEKUA JIWE KUU LA PEMBENI😂💪

Ahsanteni sana🙏”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents