Afya

Stamina na Roma watimiza ahadi yao, watoa Ventilator walizoahidi na kuzungumza haya (+ Video)

Leo tarehe 20/05/2021 #ROSTAM (Roma & Stamina) tumefanikisha zoezi la kukabidhi mashine ya kupumulia (Oxygen concentrator) na mashuka pieces 33 katika hospitali kuu ya rufaa ya mkoa wa morogoro.

Ikumbukwe mnamo mwaka jana tarehe 16/05/2020 tulianzisha challenge ya wimbo wetu wa KAKA TUCHATI tuliyooiita #RostamVentilatorChallenge na haya ndiyo matokeo yake, na leo tumefanikiwa kukabidhi kile tulichokipata kutoka kwa mashabiki wetu, na tumechagua kuleta mashine hii katika hospitali aliyozaliwa Stamina(Morogoro Regional Referral Hospital) kama sehemu ya kurudisha kwa jamii kwa support wanayotupa kwenye kazi zetu za sanaa!!

Mashine hii itaenda kusaidia sana hospitalini hapo katika masuala ya changamoto za upumuaji hasa kwa watoto wadogo, na kama unavyofahamu ukisaidia na kuokoa maisha ya watoto ni umeokoa jamii nzima.

Rostam tunatamani kusaidia jamii nzima, Rostam tunatamani kugusa maeneo mengi yenye changamoto zaidi, lakini hatuna uwezo wa kusaidia watu wote, ila tunaamini kwa kuwagusa watoto hawa (malaika) wachache itakuwa ni alama ya kuigusa jamii nzima.

Asante sana kwa mashabiki zetu na wote walioshiriki kufanikisha hili zoezi, asante kwa serikali kupitia wizara ya afya na MSD, asante kwa aliyekuwa waziri wa afya wa kipindi hicho Mh. Ummy mwalimu kwa ushirikiano mkubwa uliotupatia, Na mwisho asante kwa vyombo vyote vya habari vilivyoshiriki nasi tangu mwanzo wa challenge hii. Na mwisho akhsante kwa uongozi wa hospitali ya Morogoro kwa kupokea hiki kidogo tulichokiketa kwenu.

Tunaahidi kuendelea kurudisha kwa jamii katika kile kidogo tunachokipata kwenye muziki wetu na kuacha alama chanya kwa jamii na taifa kwa ujumla na Mungu atusimamie.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents