Michezo

Stars kusaka alama 3 leo dhidi ya Guinea

Washambuliaji waziri Junior Clement Mzize na Cyprian Kachwele wana jukumu kubwa la kuiongoza safu ya ushambuliaji ya Taifa Stars katika mchezo wa leo kuanzia saa 1:00 usiku dhidi ya Guinea utakaochezwa Uwanja wa Charles Konan Banny uliopo Yamoussoukro nchini Ivory Coast.

Guinea ambayo imeamua kutumia uwanja huo kwa mechi zake za nyumbani baada ya nchini kwao kukosa kiwanja chenye sifa kwa mujibu wa shirikisho la Soka Afrika (Caf), leo itaingia uwanjani ikiwa imetoka kupoteza kwa bao 1-0 ugenini dhidi ya DR Congo katika mchezo uliopigwa Ijumaa iliyopita pale Stade des Martyrs, Kinshasa nchini DR Congo huku Stars yenyewe ikiwa iliambulia suluhu nyumbani dhidi ya Ethiopia.

Rekodi zinaonyesha kwamba Guinea imepoteza mechi mbili mfululizo kwa matokeo ya jumla ambapo ilifunga mabao 13 na kuruhusu mawili katika kipindi cha mwezi Machi na Juni mwaka huu hivyo mchezo wa leo wataingia kwa hasira kubwa kuirekebisha rekodi yao mbovu.

Kwa upande wa Taifa Stars ambayo inaisaka Afcon ya nne tangu mwaka 1980 nayo haipo kinyonge kwani inatambua kwamba kushindwa kuondoka na pointi tatu leo itawaweka katika mazingira magumu ya kufuzu kwani hivi sasa ina point moja tu.

Stars ina kazi kubwa ya kufanya katika mchezo wa leo kwani tangu mwaka 2024 uanze imeshinda mechi tatu pekee kati ya 11 za kimashindanona kirafiki huku ikifunga mabao saba kupitia washambuliaji wanne Kelvin John, Waziri Junior, Oscar Adam na Ibrahim Hamad Hilika, wakati Simon Msuva ambaye ni kiungo mshambuliaji kama alivyo kwa ABDUL Suleiman Sopu kila mmoja akifunga goli moja sawa na beki Novatus Dismas.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents