Burudani

Studio za muziki za Bongo hazithaminiwi kama ofisi zingine – Nahreel

Mtayarishaji wa studio ya The Industry, Nahreel ambaye kwa mwaka jana (2015) alifanikiwa kutengeneza hits kubwa kumi na saba (17) amesema kuwa studio za kurekodi muziki kwa Tanzania hazithaminiwi kama ofisi nyingine.

Nahreel

Nahreel amesema kuwa mara nyingi wateja wa studio (wasanii) huwa wanapenda kufanya kazi kishikaji sana, kitu ambacho kinasababisha studio na watayarishaji wasiendelee.

“Maproducer wengi hawapati thamani….studio haipati thamani kama ofisi nyingine za kazi, kwa mfano mimi nikisema milioni moja kwa wimbo mtu anaona kama ni nyingi sana kwa production tena msanii mkubwa anaona ah nitakupaje milioni moja Nahreel si unajua si tunavyofanyaga.” Alisema Nahreel kupitia Ayo Tv.

“Hizo mi nazipataga sana kila siku na zinanishangaza sana kwanini mtu hawezi kuthamini kazi yake kwa hela ndogo kama hiyo, milioni moja is nothing Tanzania, na ukiangalia sisi (watayarishaji) tunawapa 100% royalties wasanii anapotoka na ile nyimbo pale studio anaweza kufanya nayo chochote.” Alieleza Nahreel.

Nahreel ameongeza kuwa wasanii wachanga ndio huwa wepesi kulipa wanapokwenda kufanya kazi kwenye studio yake tofauti na wasanii wakubwa ambao hutaka kutumia majina yao kufanya kazi bure.

“Wasanii wachanga wanalipa (studio) kwasababu wanakuwa in need wanakuwa wanahitaji kile kitu wanakiu na kile kitu kwahiyo watafanya chochote utakachotaka, lakaini sometime wasanii wakubwa wanakuwa wazito waziti kwasababu wanafeel kwamba brand yao inachangia na wewe kukua, kwahiyo mnaweza sometime mkakwaruzana kidogo.” Alisema Nahreel.

Ameongeza kuwa hahofii kutopata wasanii wakubwa kutaka kuja kufanya naye kazi kutokana na gharama kubwa kwasababu ameanzisha label ili atengeneze wasanii wake kwa lengo la hapo mbeleni asije kutegemea pesa za wasanii wanaokuja kurekodi.

Mpaka sasa label yake imewasaini wasanii wawili akiwemo rapper mpya wa kike Rosa Ree.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents