Burudani

Suma JKT kukusanya mirabaha ya wasanii

Taasisi ya Hakimiliki Tanzania COSOTA leo Aprili 13, 2022 imesaini makubaliano na Kampuni ya SUMAJKT Auction Mart ya kusaidia ukusanyaji wa Mirabaha kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Taarifa hiyo imetolewa leo  Jijini Dar es Salaam na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Bw. Philemon Kilaka katika Mkutano na Waandishi wa Habari.

“Mkataba huu tuliyoingia na Kampuni ya SUMAJKT  AUCTION  MART niwa mwaka mmoja na unatoa kipindi cha miezi mitatu ya uangalizi wa awali na Kampuni hii itaanza kukusanya katika Jiji la Dar es Salaam na Dodoma na kwasasa COSOTA inamawakala katika Mkoa wa Kilimanjaro na Arusha na tutae delea kuingia makubaliano,”alisema Kilaka.

Vilevile COSOTA imesema kuto kulipia Leseni ya Matumizi ya kazi za Muziki na Filamu katika maeneo ya Biashara ni Kosa kisheria na adhabu yake ni faini isiyopungua kiasi cha Tshs. 20,000,000 au kifungo kisichozidi miaka mitatu  au vyote kwa pamoja na adhabu hii ni kwa Mujibu wa Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki kifungu cha 42.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Sheria kutoka Kampuni ya SUMAJKT AUCTION MART Meja Jamal Mohamed alifafanua kuwa kazi hiyo wataifanya kwa weledi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za nchi na hakuna mabavu yatakayotumika  kwani taasisi hiyo inauzoefu wa kufanya kazi kama hizo.

“Tunafahamu umuhimu wa Wasanii kuweza kunufaika na kazi zao sababu kazi ya usanii ni kama ajira yoyote ambayo inamsaidia mtu kupata kipato na kuweza kujiendesha kiuchumi,”alisema Meja Jamal.

Aidha, COSOTA imeeleza imeamua kuchukua maamuzi hayo kwa lengo la kuweza kuongeza makusanyo ya mirabaha kwa kuweza kuyafikia maeneo mengi ili wadau waweze kunufaika na matunda ya kazi yao.

Pamoja na hayo COSOTA imefafanua kuwa inamawakala wengine katika maeneo mbalimbali nchini na kama kwa Mkoa wa Arusha na Kilimanjaro wakala wake anaitwa  Tanzania Finance Corporation.

Related Articles

Back to top button