HabariMichezo

Sura sio roho, Roho safi kama Mzamiru  Yassin 

Unapolitaja jina la kiungo wa Simba Mzamiru Yassin Selemba ‘Kiungo Punda’ kichwani inakujia picha mtu mwenye roho mbaya kutokana na aina yake ya ufanyaji kazi kiwanjani ndiyo maana wakamuita kiungo Punda kazi ya Punda ni kufanya kazi ngumu kubeba mizigo kama Mzamiru anavyo wakabia wakina Chama pale Simba yupo fiti sana ana misimu 6 mpaka sasa ndani ya Simba na anacheza na mara zate anaitwa timu ya taifa bila kukosekana

Msimu uliopita Mzamiru akiingia katika kitengo cha kugombea kiungo Bora wa Ligi kuu hiyo ni kuonesha ubora wake na kusibitisha ubora wake kwa sasa lakini ukiacha sifa zote nilizokutajia hapo Mzamiru Yassin ndani ya familia yake ukiwauliza wakuelezee Mzamiru hawatakwambia kuhusu kiungo Punda watakwambia ndiyo mwanadamu mwenye roho nzuri na upendo zaidi kuwahi kutokea ni mtu ambaye anakumbuka alipotoka pamoja na kulipa fadhila kwa ndugu zake hasa baba yake Mdogo Selemba ambaye amelea pale Morogoro alipotoka Kigoma na kumsomesha pamoja na kumsimamia katika mambo ya mpira mpaka Leo kiungo Punda amefikia malengo yake.

Mzamiru Yassin Selemba baada ya kufanikiwa kwanza amewajengea nyumba kubwa ndugu zake kwaajili ya kukaa pia akawaita na kuwauliza anataka awafanyie Nini ndugu zake Vijana wapo wanne Tena siyo wa tumbo moja wakasema wanataka Bajaji Mzamiru akanunua Bajaji nne mpya Tena kutoka Dar akazipakia mpaka Moro kuwapeleka ndugu na baba yake Mdogo kamfungulia biashara tofauti tofauti pamoja na kusimamia miradi ya Mzamiru kama Mashamba makubwa ambayo Mzamiru analimisha Nyanya uko tuliani Morogoro.

NB:Mzamiru kwao wamezaliwa 12 kwahiyo kule Kigoma wanatimu ya mpira ya familia mpaka babake mzazi Fundi,unaambiwa katika kikosi Cha familia yeye ndiyo hajui mpira.

By Issaya Dede

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents