Technology

Taarifa hii nzuri ikufikie wewe mtumiaji wa Simujanja ‘Smartphone’ hapa Tanzania kwa mwaka 2020

Toleo jipya la simu CAMON 12 Pro ya hivi karibuni imewekewa kitufe cha Msaidizi wa Google (Google assistant) ambacho kinaruhusu watumiaji kufanya mambo mengi zaidi kwenye mfumo wa Google.

Kampuni kinara ya Kimataifa ya simu za rununu ya TECNO yenye simujanja yake ya Camon 12 Pro ya hivi karibuni, inayowezeshwa na mfumo wa uendeshaji wa Pie ya Google (Google’s Android™ 9 Pie operating system), imeweka kitufe cha Msaidizi wa Google (Google assistant) kwenye CAMON 12 Pro katika mkutano wa maonesho ya teknolojia ya mwaka 2020 Januari hii.

TECNO imejiunga na kuwa mshirika wa Google kuleta mfumo mpya wa uendeshaji kwa wateja wake.

Wakati Google inafanya maboresho ya mfumo endeshi (Android) kwaajili ya kuleta ufanisi madhubuti kwenye vifaa janja vipya vya kisasa, TECNO ilizindua simu mpya ya kisasa ya CAMON 12 Pro kwa kuweka Kitufe cha Google assistant ambayo ilioneshwa kwenye kibanda cha Google katika mkutano wa maonesho ya teknolojia 2020 ili kusaidia watumiaji kufanya mambo kwa haraka zaidi na kupangilia vitu muhimu kwenye ratiba ambavyo vinavyoweza kufanyika baadaye.

Google ikionesha Simujanja zenye kitufe cha Google Assistant kwenye banda lake katika mkutano wa maonesho ya teknolojia 2020.

TECNO CAMON 12 PRO yenye Kitufe cha Google Assistant kama ilivyooneshwa kwenye kibanda cha Google.

“TECNO inawasisitiza watumiaji wake kujihusisha kikamilifu na matumizi ya vifaa vyake na programu za ndani,” alisema Stephen HA, rais wa TRANSSION na Mkurugenzi Mtendaji wa TECNO “Tunafurahi kuanza ushirikiano huu na Google.”

Simu hii mpya ya CAMON 12 Pro ina kamera tatu nyuma ambazo zina 16 + 2 + 8MP AI Max Triple, pia ina mapinduzi ya kuonyesha-alama ya kidole kwenye skrini na mfumo wake wa uendeshaji yaani Android™ Unasaidia kufanya yafuatayo:

● Multi-camera support na camera updates: Kwa kamera zake tatu za nyuma, mtumiaji hufurahia picha iliyokuzwa isiyo na ukungu, atafurahia pia bokeh na mwonekano sawia wa picha.

● AR Emoji: Watumiaji wa CAMON 12 Pro wanaweza kuboresha emoji zao wanazopenda na mwonekano halisi wa uso.

● Matumizi ya Meseji Yaliyoboreshwa: Watumiaji wanaweza kujibu ujumbe au kuingiza maandishi mengine mapya moja kwa moja kutoka kwenye arifa (notifiction). Mfumo endeshi ambao ni Android ™ 9 Pie ndani ya CAMON 12 Pro sasa una uwezo wa kuonesha picha kwenye Arifa za Kutuma ujumbe katika simu.

● Mpangilio wa mkondo arifu uliorahisishwa: Watumiaji wanaweza sasa kuzuia makundi (groups) yote katika mipangilio ya arifu kwenye app. Android ™ 9 Pie sasa inatuma taarifa au hutoa kiashiria wakati hali ya kuzuia makundi kwenye arifu inapobadilika.

● Kitufe cha Google Assistant: Ukiwa na Google Assistant, watumiaji wanaweza kudhibiti kazi, kuwasiliana, kupata majibu ya wanachouliza na kudhibiti mienendo ya nyumbani popote uendapo. Pia husaidia watumiaji kupangilia mambo yao ya kufanya baadaye, kuhifadhi kazi za kufanya baadaye na kukumbushwa na Google Assistant wakati wa kuzifanya unapokuwa umefika moja kwa moja kwenye skrini ya simu. Ili kuanza, sema tu “Halo Google” au bofya Kitufe cha Google Assistant.

TECNO imeonesha uwezo wake mkubwa kwa kuongoza na kwenda sambamba na mahitaji ya watumiaji wake katika kutimiza kiu ya teknolojia mpya kabisa inayotamba kwa sasa kulingana na tafiti na Maendeleo.

TECNO itaongeza zaidi ushirikiano wake na Google ili kuwapa wateja huduma nzuri zaidi na simu za kisasa zenye teknolojia ya juu kabisa.

Kuhusu Kampuni ya Simu ya TECNO

Kampuni ya Simu ya TECNO ni kampuni tanzu kinara na bora kutoka TRANSSION Holdings. Ikienda kwa kaulimbiu yake ya “Expect More” yaani Tarajia Zaidi, TECNO imejizatiti kikamilifu kuwapa watu simu za kisasa zenye teknolojia ya juu kwa bei wanayoweza kuimudu pia TECNO imedhamiria kuruhusu watumiaji kuvuka mipaka yao ya sasa na kugundua ulimwengu mpya wenye fursa zinazowezekana.

TECNO inaelewa mahitaji ya watumiaji kutoka katika masoko tofauti na inawapa uvumbuzi wa vifaa mbalimbali vya mawasiliano zikiwemo simujanja, tablets na simuvitochi.

TECNO ni Kampuni Kubwa ya Kimataifa na ipo katika masoko yanayoinukia zaidi ya 60 kote ulimwenguni. Pia ni Mshirika rasmi wa Kimataifa wa Klabu ya Mpira miguu ya Manchester City.

Je, una maoni gani kuhusu teknolojia hii?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents