Habari

Taasisi zilizo chini ya waziri mkuu zaagizwa ushirikiano na vyombo vya sheria (+Video)

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu), Andrew Massawe, ameziagiza Taasisi chini ya Wizara hiyo kuvihusisha vyombo vya sheria katika kutekeleza majukumu yao ili kuleta usawa na uwajibikaji miongoni mwa Taasisi husika na wadau wao.

Maagizo hayo ameyatoa alipofunga semina kuhusu Sheria ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi Na. 5 ya mwaka 2003 ambayo ilitolewa na OSHA kwa Mawakili wa Serikali chini ya Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP).

Akifungua semina hiyo, Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA,Khadija Mwenda, amesema lengo la semina hiyo ni kujenga uelewa wa pamoja baina ya OSHA na Mawakili wa Serikali ili kurahisisha utekelezaji wa Sheria husika.

Baadhi ya Mawakili wa Serikali walioshiriki katika semina wakiwemo Adolf Verandumi, Mkunde Mshanga na Esther Chale wameishukuru Taasisi ya OSHA kwa kuandaa mafunzo hayo. Aidha, wameeleza kuwa kupitia mafunzo hayo wamejifunza mambo mengi ambayo yatawasaidia katika kusimamia mashauri yanayohusu masuala ya Usalama na Afya mahali pa kazi.

Taasisi hizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) ni pamoja na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Idara ya Kazi, Tume ya Uamuzi na Usuluhishi (CMA), Mfuko wa Hifadhi kwa Jamii wa Sekta Binafsi (NSSF), Mfuko wa Hifadhi kwa Jamii wa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents