Michezo
Tabora yawa kinara wa kukimbiza makocha

TANGU msimu huu umeanza, Tabora United imefundishwa na makocha wanne hadi sasa ndiyo kinara kati ya timu zote 16, zinazoshiriki Ligi Kuu Bara, baada ya kuanza na Mkenya Francis Kimanzi aliyeondoka Oktoba 21, 2024, kutokana na matokeo mabaya.
.
Baada ya Kimanzi, akafuata Mkongomani Anicet Kiazayidi aliyeondoka pia Machi 28, 2025, huku nafasi yake ikichukuliwa na Mzimbabwe Genesis ‘Kaka’ Mangombe aliyedumu hadi Aprili 18, 2025, kisha Simonda Kaunda, raia wa Zambia kurithi mikoba.