Michezo

Taifa la Senegal latangaza mapumziko baada ya kushinda ubingwa wa AFCON

Rais wa Senegal Macky Sall ametangaza Jumatatu kuwa siku ya mapumziko kusherehekea ushindi wa timu ya taifa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon).

Rais ambaye alikuwa nje ya nchi amefutilia mbali awamu ya mwisho ya safari yake ili kuwakaribisha nyota hao wa soka kurejea nchini siku ya Jumatatu.

Senegal ilishinda fainali ya kwanza ya Afcon baada ya kushindwa mara mbili katika fainali mwaka 2002 na 2019.

Waliishinda Misri 4-2 kwa mikwaju ya penalti na kupata ushindi wao baada ya fainali kumalizika bila bao kufuatia muda wa nyongeza.

Wakati huo huo, raia wameendelea kusherehekea usiku kucha kuamkia Jumatatu katika miji mbalimbali nchini Senegal kufuatia ushindia wa Kombe la Mataifa ya Afrika.

Video zinaonesha mashabiki wa timu hiyo wakiwa wanapeperusha bendera ya taifa hilo wakiwa wanacheza densi pamoja na ujumbe kutoka kila pembe uliokuwa unamiminika kwenye mitandao ya kijamii.

Msisimko huo haukuweza kufichika hata katika sehemu za burudani. Kwenye barabara mbalimbali, watu walisherehekea ushindi huo kwa aina yake

Senegal iliishinda Misri kwa mikwaju ya penalti 4-2 na kutwaa ushindi wa kwanza wa Afcon baada ya kushindwa mara mbili katika fainali zilizopita.

Kocha Aliou Cissé ambaye kama mchezaji alikosa penalti muhimu katika kushindwa kwa fainali ya 2002 na alikuwa kocha wakati timu hiyo iliposhindwa katika fainali miaka mitatu iliyopita alisifiwa mtandaoni. Senegal na Misri zitakutana tena katika mechi nyingine mwezi ujao kwenye mchujo wa kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents