Fahamu

Taifa linalofanya mazishi ya watu wenye Corona kwa siri usiku, Kupunguza maambukizi

Marufuku iliyowekwa nchini Afrika Kusini dhidi ya mikusanyiko ya watu mazishini imelazimu watu kuachana na tamaduni nyingi lakini pia imesaidia kuvumbuliwa kwa tamaduni zingine za jadi ikiwa ni pamoja na, “mazishi ya kisiri”, kama alivyogundua mwandishi wa BBC Pumza Fihlani akiwa mjini Johannesburg.

Ilichukuwa mazishi moja kusababisha watu 40 kuambukizwa virusi vya corona.

Mnamo Machi 21, chini ya wiki moja baada ya rais Cyril Ramaphosa kutangaza corona kuwa janga la kitaifa na kupiga marufuku mikusanyiko mikubwa ya watu ili kudhibiti kueneza kwa virusi vya corona, karibu watu 100 walihudhuria mazishi katika kijiji cha Majola, katika eneo la Cape Mashariki.

Kijiji hicho cha mashambani cha AmaMpondomise, sasa ni kitovu cha ugonjwa wa corona katika eneo hilo.

Mazishi iliyofanyika Machi 21 March, pamoja na zingine mbili katika eneo la Port Elizabeth, imechangia watu 200 kupatikana na ugonjwa waCovid-19 katika mkoa huo – ikiwa ni robo ya watu wote watu wote.

Kupuuza mamlaka

Hali ilivyo kwa sasa mamlaka imeruhusu watu, 50 pekee kuhudhuria mazishi, lakini idadi hiyo ni kidogo katika baadhi ya maeneo.

Msemaji wa kitengo cha afya katika eneo la Eastern Cape, Sizwe Kupelo anasema baadhi ya familia zimekuwa “zikipuuza” agizo la mamlaka la kudhibiti mambukizi ya corona, hali ambayo imechangia kuongezeka kwa visa vya maambukizi.

“Tunahofia sana kuhusu mwenendo wa mazishi katika mkoa huu,” Bw. Kupelo alinukuliwa akisema katika runinga ya News24.

“Tumekaribisha mapendekezo yaliyotolwa na viongozi wa kijamii kwa waziri wa Afya kuhakikisha watu wote waliofiliwa kupewa maelekezo sawa; kama vile, usafiri wa moja kwa moja kutoka mochari hadi kaburini.”

Women sitting for a funeral

Lakini ni vigumu kubadilisha baadhi ya tamaduni za jadi na bado kumekuwa na ripoti ya mikusanyiko mikubwa ya watu mazishini

“Mazishi, sawa na harusi ni sherehe ya kitamaduni katika baadhi ya jamii na hutumiwa kuadhimisha, tukio muhimu katika maisha ya mtu aliyefariki,” anaeleza mtaalamu wa masuala ya kitamaduni Profesa Somadoda Fikeni.

“Waafrika wanazingatia utamaduni huo kama njia ya kuwafariji walipatwa na msiba ili kudumisha mshikamano katika jamii.

Kila mmoja anatoa heshima zake za mwisho

Kwa Jamii nyingi ya Waafrika nchini Afrika Kusini, mazishi hujumuisha tamaduni za Kiafrika zilizochanganyika na tamaduni za Kikristo.

Familia inapopatwa na msiba, watu husafiri kutoka maeneo mbali mbali kuhudhuria mazishi na kusalia mazishini kwa siku kadhaa hadi matambiko ya kuondoa msiba yafanyike.

Safari hizo hufanyika mara kwa mara nyumbani kwa waliofiliwa ambapo wageni huja kutoa pole zao kuwafariji na vil evile kuwasaidia kwa maandalizi ya matanga.

Mifugo huhitajika kuchinjwa ili kuwalisha wageni wengi wanaotarajiwa kufika msibani, kunahitajika kupikwa, hasa karibu na mahali kuliko msiba, na katika maeneo ya vijijini, kaburi linahitaji kufukuliwa, mara nyingine watu hutumia vifaa sawa kusaidiana kufukua kaburi.

Wale wanohudhuria mazishi mara nyingine hawajulikani na familia ya marehemu lakini milia ilivyo hkauna mualiko msibani.

Huenda wakawa ni washirika wa kanisha la kijiji hicho, au hata wapita njia ambao wamepokea taarifa za msiba na wanataka kuungana na familia iliyofiwa ili kuwafariji kipindi hicho kigumu.

Kila mmoja anakaribishwa.

Mfumo wa usambazaji wa virusi

Siku ya maziko, mamia ya watu hukusanyika kwa ibada ya kanisa, wakiwa wamekaribiana. Shughuli ya siku ikiendelea watu katika jamii husaidiana kuwapa chakula mamia ya waombolezaji waliofika. Na wageni hula pamoja, tena wakiwa wamekaribiana.

“Maambukizi ya virusi katika mazingira hayo ni ya hali ya juu ,” anaonya Bw. Fikeni.

Katika juhudi ya kupata njia mbadala ya watu kuwazika wapendwa wao, Mgalme wa AmaMpondomise King Zwelozuko Matiwane alipiga marufuku ibada zote za mazishi katika eneo lake na kuzindua mfumo wa jadi wa maziko unaofahamika kama ukuqhusheka, ma mazishi ya kisiri.

A crucifix headstone

South Africa funeral regulations

In the time of coronavirus

  • Maxiumumof 50 people allowed at a funeral
  • All night vigilsare prohibited
  • Only those closeto the deceased are allowed to travel for the funeral
  • Social distancingmust be observed during the ceremony

Source: South Africa government

Presentational white space

Msemaji wake Nkosi Bhakhanyisela Ranuga, anasema hatua hiyo ilifikiwa baada ya viongozi wa kijamii katika eneo hilo kushauriana.

“Tunajaribu kuwalinda watu dhidi ya janga hili.

“Tunapofuata utamaduni huu [wa ukuqhusheka] inamaanisha watu wanaombwa kuzika siku hiyo ama siku inayofuata na watakaoruhusiwa kuzika ni wale walikuwepo nyumbani wakati msiba ulipotokea,” aliambia BBC.

Sherehe ya kutakasa

Ufalme wa AmaMpondomise unajumuisha miji minne ya , Qumbu, Tsolo, Ugie na Maclear, na vijiji vilivyopo karibu.

“Kwa kurejesha utamaduni huu wa kala inamaanisha ni familia ya karibu ya marehemu pekee itakayoruhusiwa kumzika aliyefariki.

Baada ya mazishi, familia itaweza kufanya shere za kutakasa mji baada ya kurejea kutoka makaburini,” anaeleza Bw. Ranuga.

Sherehe hizi hufanywa kupitia ibada maalum ya kusafisha mji na familia dhidi ya “wingu la giza la kifo”.

Kawaida ni mambo ya kibinafsi na familia ya karibu pekee.

Mchungaji akiongoza mazishiMchungaji akiongoza mazishi

Katika juhudi ya kusaidia kuzuia kuenea kwa virusi vya corona, baadhi ya watu wanaunga mkono kurejelewa kwa utamaduni wa ukuqhusheka kwasababu ya kiwango cha chini cha fedha ambacho familia itatumia kugharamia ya mazishi, hasa nyakati hizi ngumu za kiuchumi.

“Familia huingia madeni makubwa kuzika wapendwa wao siku hizi,” Nosebenzile Ntlantsana, kiongozi wa kijamii anasema .

“Kama viongozi wa kijamii tanahitajka wakati mwingine kuingilia kati kutatua mzozo kati ya familia na watu waliotua huduma wakati familia inaposhindwa kulipa deni. Inasikitisha kuona jinsi watu wanavyopambana kufanya shere kubwa ya mazishi siku hizi – pengine utamaduni huu utasaidia familia katika jamii yetu.”

Ibada ya mazishi imebadilika kutaka shughuli ya siku nzima hadi ibada ya lisali moja nyumbani kwa waliofiwa huku wanaohudhuria ikiwa ni watu 50, na wanofika kaburini ni watu 25 ama wachache kuliko hao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents