Taitra kuhamasisha ulinzi na utunzaji mazingira Afrika

Baraza la Maendeleo ya Biashara ya Nje la Taiwan, TAITRA limezindua kampeni inatoa wito kwa wafanyabiashara wanaozingatia mazingira kote barani Afrika kutuma maombi yao ya kupata nafasi ya kujishindia zawadi ya kuendeleza ubunifu katika bidha zinazohamasisha ulinzi na utunzaji wa mazingira
Shindano hilo linalofahamika kama “Go Green with Taiwan” linalenga kutambua na kusherehekea bidhaa za kisasa ambazo ni rafiki wa mazingira na suluhisho linazoweza wa kuleta mchango i chanya kwa kulinda na kutunza mazingira katika maeneo mbalimbali ulimenguni
Mradi wa “Go Green with Taiwan” Unatafuta nini?
Mradi unatafuta mapendekezo ambayo yanashughulikia changamoto mbali mbali za mazingira, pamoja na:
(1) Kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
(2) Nishati mbadala na ufanisi wa nishati
(3) Udhibiti endelevu wa taka
(4) Kuzuia na kudhibiti uchafuzi
(5) Usafiri endelevu.
Ili kushiriki shindano hilo mfanyabiashara mlengwa wa bidha zinazochochea na kuhamasisha utunzaji wa mazingira atapaswa kufuata hatua zifuatazo:-
Hatua ya 1: Waombaji watahitaji kuwasilisha pendekezo fupi linaloelezea bidhaa zao rafiki wa mazingira au suluhisho la utunzaji wa mazingira.
Hatua ya 2: Waombaji walioorodheshwa wataalikwa kuwasilisha pendekezo la kina zaidi na kushiriki katika kikao kwa njia ya sauti.
ZAWADI: Washindi 3 bora wa shindano la “Go Green with Taiwan” watapokea kifurushi cha zawadi ambacho kinajumuisha: fedha taslim Dolar za kimarekani elfu ishirini (USD 20,000) na safari iliyofadhiliwa kikamilifu hadi Taiwan kwenda kushiriki hafla ya tuzo; na kupata Ushauri kutoka kwa wataalam wa tasnia; Usaidizi wa uuzaji na utangazaji wa bidha hizo
Jinsi ya Kutuma Ombi: Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha mapendekezo ni tarehe 31 Agosti 2024. Kwa maelezo zaidi kuhusu shindano hilo na jinsi ya kutuma ombi, tafadhali wasiliana na waandaaji.
TAITRA iliyoanzishwa mwaka wa 1970, ni shirika kuu la Taiwani lisilo la faida linalokuza biashara likiifadhiliwa na serikali na mashirika ya viwanda, TAITRA husaidia makampuni katika kupanua wigo wao wa kimataifa.
UNAWEZA KUJISAJILI SASA KUPITIA LINK HII >> This is the right link: https://go-green.growthpad.co.ke/