TAKUKURU yawabamba watumishi 23 wa MOI waliokuwa wanataka kuipiga tsh 1.2 Bilioni (Video)

Watumishi 23 wa Idara ya Famasia katika Taasisi ya Mifupa (Moi) wanachunguzwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa madai ya wizi wa dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya Sh1.2 bilioni. Hayo yameelezwa leo Jumatano Januari 13, 2021 na mkurugenzi mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo katika mkutano wake na waandishi wa habari.

 

Mbungo amesema watumishi hao wanadaiwa kufanya udanganyifu huo kati ya mwaka 2018 hadi 2020.

Akielezea namna ubadhirifu huo ulivyofanyika, Mbungo amesema, watuhumiwa hao walikuwa wanaandika taarifa za uongo katika mfumo unaofahamika kama MEDPRO4 kwa kuweka idadi kubwa ya vifaa vilivyotolewa tofauti na idadi halisi iliyotolewa na madaktari kwa wagonjwa na wateja.

Related Articles

Back to top button
Close