Michezo

Takwimu za kocha Nabi, Yanga 2021/22 ni kiwango cha ‘Dunia ya kwanza’

Moja kati ya kitu kikubwa ambacho Mabingwa Kihistoria Ligi Kuu soka Tanzania Bara Young Africans Sports Club wamefanikiwa katika msimu wa 2021/2022 ni kumpata Kocha, Nasreddine Mohammed Nabi.

Nabi ameleta mabadiliko makubwa sana ndani ya kikosi cha Yanga na ameifanya timu hiyo kuwa yenye ushindani wa kweli kunako Ligi Kuu soka Tanzania Bara, bila kumung’unya maneno, uwepo wake Jangwani kumeleta ugumu kwa timu nyingine kupata alama tatu zinapokutana na Wananchi hao.

Yanga ya Nabi imekuwa ya moto kweli kweli msimu huu, kukutana na Yanga hii lazima uwe umejipanga hasa, kama kwenye benchi yupo Mtunisia huyu.

Uhitaji elimu ya Chuo Kikuu ‘PHD, Masters, wala Degree’ kuona ubora wa Prof. Nabi ndani ya Yanga bali ‘Statistics’ (takwimu) zake za kutisha zinatosha kuona umuhimu wake kwa Young Africans Sports Club.

Na hizi ni takwimu za Yanga msimu huu chini ya Kocha, Nabi amesimamia jumla ya michezo 46.

Ameshinda Michezo 33

Amefungwa Michezo  4

Sare Michezo 9

Magoli yakufunga jumla 72

Magoli ya kufungwa 23 na Clean Sheet 25, hizi ni takwimu za mashindano yote NBC,  FA, CECAFA, KIMATAIFA, MAPINDUZI NA KIRAFIKI.

NBC PREMIER LEAGUE MSIMU HUU KAONGOZA MICHEZO 20

Ameshinda Michezo 17

Ametoa Sare Michezo 3

Magoli yakufunga jumla 35

Magoli yakufungwa 6, goal difference 29 na Clean Sheet mechi 14.

AZAM SPORTS FEDERATION CUP MICHEZO 4

Ameshinda Michezo 3

Ametoa Sare Michezo 1

Magoli yakufunga jumla 35

Magoli yakufungwa 2, Clean Sheet 2

MAPINDUZI CUP MICHEZO 3

Ameshinda Michezo 2

Ametoa Sare Michezo 1

KAGAME CUP MICHEZO 3

Ametoa Sare Michezo 2

Amefungwa Michezo 1

CAF Mechi mbili na zote amefungwa

MECHI ZA KIRAFIKI MICHEZO 13

Ameshinda Michezo 11

Amefungwa Michezo 1 (Zanaco)

Ametoa Sare Michezo 1

Magoli yakufunga jumla 22

Magoli yakufungwa 9, Clea Sheet michezo 6.

Aprili 20, 2021 Young Africans ilimtambulisha, Nasreddine Mohammed Nabi kuwa Kocha Mkuu kwa kandarasi ya Mwaka mmoja na Nusu akipokea kijiti cha Cedric Kaze.

Aliisimamia michezo nane (8) ya mwisho wa msimu wa Ligi akishinda mitano (5), kufungwa mmoja na Azam, Sare mbili. Na FA mechi mbili (2) akishinda Nusu Fainali na Biashara United na kufungwa mmoja Fainali na Simba SC hivyo Jumla tangu kujiunga Yanga Kwa ujumla ana Mechi 56.

IMEANDIKWA NA @fumo255

Related Articles

Back to top button