Habari

Tamasha la kihistoria kufanyika Kivule

TAASISI ya Sunshine kwa kushirikiana na Jukwaa la wanawake Tanzania inatarajia kufanya kufanya tamasha kubwa la kuwakutanisha wanawake kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kushirikishana fursa zilizopo Kitaifa, Kimkoa, Kiwilaya, Kata na njia ya kuzifikia.

Akizungumzia tukio hilo la kihistoria Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Kivule, Mwalimu Nuru Sudi alisema kwa Umoja wao wanatarajia kufanya hivyo Septemba 14 mwaka huu na wanawakaribisha wanawake wote.

Alisema lengo ni kushirikishana fursa mbalimbali, kupitia wanawake waliofanikiwa ambao ni chachu ya mafanikio kwa wengine.

“Wanawake waliofanikiwa watakuwa msukumo wa kuwainua wengine kwa kuwa nguvu ya kupambana ipo kinachokosekana ni kutojua njia ya kupitia.

“Wenzetu waliofanikiwa pamoja na viongozi watatuelekeza fursa zetu ambazo zipo Kitaifa, Kimkoa, Kiwilaya, Kata na njia ya kuzifikia hizo fursa,”alisema Mwalimu Sudi.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Kivule, Mwalimu Nuru Sudi akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo na Diwani wa Kata ya Kivule, Nyansika Montena katika uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Kivule

Alisema wanawake pia watapatiwa elimu ya malezi, ndoa, Uchumi na masuala ya Jamii na hayo yote yatafanyika katika Ukumbi wa Lukolo uliopo Kitunda relini.

“Wanawake Kivule wameona malezi ya watoto sasa hivi ni changamoto kutokana na utandawazi hivyo wakaona kupitia mkusanyiko huo tukumbushane namna gani tunaweza kulea watoto wetu,”alisema.

Hata hivyo alisema kutakuwa na gharama za kuchangia ili kufanikisha tukio hilo.

Aliainisha kwamba gharama za kuchangia Sh 50,000 kawaida, Sh 100,000 VIP na Sh 600,000 meza ya watu 10.

Alisema washiriki watapata kitenge, chakula, vinywaji na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali maarufu.
“Nawakaribisha wadau wote wanaotaka kushiriki kwa njia mbalimbali, wadhamini wanahitaji kutangazanbiashara zao katika siku hiyo muhimu wote wanakaribirishwa,”alisema.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents