BurudaniHabari

Tamthilia inayohusu maisha ya utapeli ya Hushpuppi inaandaliwa na 50 Cent

Msanii maarifu wa muziki wa rap wa Marekani 50 Cent ametangaza kuwa anatengeneza msururu wa vipindi vya televisheni kuhusu maisha ya mfungwa -tapeli sugu Mnigeria na mshawishi wa mtandao wa Instagram, Hushpuppi.

Tangazo hilo la 50 Cent limezua mjadala mtandaoni huku baadhi wakiunga mkono wazo hilo, huku wengine wakisema utawafanya Wanigeria waonekana vibaya.

Akituma ujumbe huo kwenye ukurasa wa Instagram, 50 Cent ambaye jina lake halisi ni Curtis Jackson, alisema kuwa ilimbidi afanye hivyo: “Kwa jaili ya walaghai wangu ni lazima nifanye hili, Msururu wa Hushpuppy unakuja karibuni! (Hushpuppy series coming soon !)”

Msanii huyo wa muziki wa rap ana historia ya kuandaa vipindi vya TV, ikiwa ni pamoja na msururu wa maigizo wa Power, ambao kwa mara ya kwanza ulianza kutangazwa mwaka 2014.

Hushpuppi, ambaye jina lake halisi ni Ramon Abbas, kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka 11 jela kwa mchango wake katika mtandao wa kimataifa wa utapeli.

HUSHPUPPI/INSTAGRAM

Huspuppi alikuwa maarufu kwenye mtandao wa Instagram ambao aliutumia kuonyesha utajiri wake mkubwa kwa wafuasi wake milioni 2.8 ,hadi alipokamatwa mjini Dubai mwaka 2020, na akaunti yake kufungwa.

Kwenye mtandao wa Twitter baadhi ya watu wanaonyesha furaha yao juu ya mpango wa 50 Cent: “Nasubiri kwa hamu kuona ni nini 50 Cent atatupatia kuhusu hili !”mtu mmoja alisema.

Mwingine anasema50 Cent anapaswa “Kuipiku Nollywood kwa hili”.

Hatahivyo,Wengine wameelezea kutofufahishwa kwaona hili, huku mmoja wao akituma ujumbe akisema : “kwanini usitazame karibu yako na kuandaa msururu wa kitu ambacho kinaongelea jambo chanya kuhusu Wanigeria, kwani kuna mengi yanayokuzingira na kote duniani”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents