Habari
Tangazo la nafasi za Ajira lakanushwa na Asas
Kampuni ya Uuzwaji na usambazaji wa Maziwa nchini ‘Asas Group of Companies’ imekanusha juu ya taarifa iliyokuwa ikisambaa mitandaoni kuhusu nafasi za Ajira.
‘Tumebaini kuwepo kwa Tangazo la ajira linalosambazwa kupitia kwa njia Kama mitandao ya Kijamii, barua Pepe, tovuti zisizo rasmi, likidai kuwa limetolewa na kampuni ya Asas’
‘Tungependa kufafanua kwamba tangazo hilo ni la Uongo (Feki) na halijatolewa na Asas of Group Companies kampuni zetu hazina uhusiano wowote na tangazo na hazifanyi mchakato wowote wa ajira kama inavyodaiwa, Tunatoa wito kuwa umma kuupuza tangazo hilo na tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza’