Tanzania 3 -2 Madagascar, goli la Feisa Salum laibeba Stars hadi nafasi ya kwanza ya group J

Tanzania imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 3 – 2 dhidi ya Madagascar na hivyo kuongoza group J kwa alama nne (4).


Benin wakishika nafasi ya pili kwa alama nne (4) ikiwa ni tofauti ya magoli tu dhidi ya Tanzania.

Nafasi ya tatu ikikaliwa na DR Congo wenye point mbili mpaka sasa na timu ya Madagascar ikiburuza mkia pasipo alama hata moja mpaka sasa.

Hii ikiwa ni mechi ya kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.

Mechi ijayo Tanzania itawakaribisha Benin kwa Mkapa Oktoba 6, na kama itawafunga basi itazidi kujikita kileleni mwa msimamo wa kundi J.

Magoli ya mchezo huo yamefungwa na Nyoni 2’ (P), Miroshi 26’, Feisal 52’ Rakotoharimalala 36′, Fontaine 45’

Related Articles

Back to top button