Habari

Tanzania kuzalisha mabaharia wengi wenye ujuzi

Mwakilishi kutoka Tanzania Shipping Agencies Corporation TASAC  ameipongeza DMTA kwa juhudi zake za kukuza mafunzo ya ubaharia nchini. Amesema TASAC itaendelea kushirikiana na chuo hicho ili kuhakikisha Tanzania inazalisha mabaharia wengi wenye ujuzi na kukidhi mahitaji ya soko la kimataifa.

Ameeleza kuwa kwa sasa duniani kuna upungufu mkubwa wa mabaharia, hali inayofungua fursa kwa vijana wengi kujiunga na taaluma hiyo na kupata ajira katika sekta ya usafiri wa majini duniani.

Kwa upande wake, Mkuu wa DMTA, Capt. Ken Chimwejo amesema Tanzania kwa sasa inachangia chini ya asilimia 1 ya mabaharia wote duniani, jambo linaloonyesha bado kuna uhitaji mkubwa wa wataalamu katika sekta hiyo.

Ameongeza kuwa takribani asilimia 90 ya bidhaa zote duniani husafirishwa kupitia njia za maji, hivyo ubaharia ni sekta muhimu sana kwa uchumi wa dunia.

Takwimu hizi zimetolewa jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa chuo cha kwanza binafsi cha mafunzo ya ubaharia nchini – DMTA, ambacho kinalenga kuwajengea vijana uwezo unaokidhi viwango vya kitaifa na kimataifa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents