Michezo

Tanzania yapanda Viwango FIFA

Timu ya taifa ya Kenya ya mpira wa miguu Harambee Stars imeshuka kwa nafasi mbili katika viwango vya hivi punde vya Fifa vilivyotolewa Alhamisi na shirikisho hilo la soka duniani.

Timu ya taifa ya kandanda sasa iko katika nafasi ya 108, chini kutoka nafasi ya 106 iliyokuwa nayo Oktoba.

Kushuka huku kumefuatia kushindwa kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika 2025 huku Kenya ikishindwa kupata tiketi ya kushiriki michuano hiyo yenye hadhi ya juu zaidi barani.

Stars ilimaliza ya tatu katika Kundi J nyuma ya Cameroon na Zimbabwe kufuatia sare ya 1-1 dhidi ya timu ya taifa ya Namibia na sare tasa dhidi ya Namibia katika mechi mbili za mwisho za kufuzu mapema mwezi huu.

Timu hiyo pia ilitwangwa mabao 2-0 na kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Sudan Kusini katika mchezo wa awamu ya kwanza ya kuwania kufuzu ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) ingawa Kenya tayari imefuzu kushiriki michuano hiyo ikiwa ni mwenyeji pamoja na Tanzania na Uganda.

Uganda imesalia na nafasi yake ya juu zaidi katika ukanda wa Cecafa licha ya kushuka kwa nafasi moja hadi 88 huku Morocco ikisalia kuwa nchi iliyo juu zaidi barani Afrika katika nafasi ya 14.

Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi zilizofanya vyema katika viwango hivyo kwani iliruka nafasi sita kutoka nafasi ya 112 hadi 106, hatimaye kuipita Kenya.

Taifa Stars itaelekea Morocco mwaka 2025 baada ya kushikilia nafasi ya pili katika Kundi H baada ya kushika nafasi ya pili nyuma ya DR Congo katika mchujo.

Argentina inasalia kuwa kikosi kinachoongoza juu kwenye viwango vya FIFA, huku Ufaransa na Uhispania zikihifadhi nafasi zao katika nafasi ya pili na ya tatu mtawalia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents