Habari

Tanzania yawakaribisha wawekezaji wote wa madini mkakati

Waziri wa Madini,  Anthony Mavunde amesema Tanzania inakaribisha wawekezaji wote wa madini mkakati na kuweka msisitizo kwamba uongezaji thamani wa madin hayo mkakati lazima ufanyike Tanzania.

Mavunde ameyasema hayo leo Bali,Indonesia wakati wa majadiliano juu ya manufaa ya Madini Mkakati katika kukuza uchumi wa nchi wazalishaji ikiwa ni sehemu ya mkutano wa jukwaa la Idonesia Afrika.

Waziri Mavunde ameonesha dhamira njema na mazingira mazuri yaliyowekwa na serikali chini ya uongozi wa Dkt. Samia S. Hassan kuvutia uwekezaji nchini na hivyo kuwakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza katika uchimbaji wa madini mkakati ambayo yana mahitaji makubwa duniani na Tanzania imebarikiwa nayo.

Waziri Mavunde alisisitiza kuwa kwa sasa ni sharti la lazima kwamba madini mkakati hayo yaongezwe thamani nchini ili kuvutia viwanda vya kutengeneza bidhaa mbalimbali zikiwemo betri ya magari ya umeme.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents