Michezo

Tanzia: Mino Raiola wakala wa Paul Pogba, Erling Haaland afariki Dunia

Mino Raiola wakala maarufu wa katika ulimwengu wa mchezo wa soka raia wa Italia afariki dunia nyumbani kwao akiwa na umri wa miaka 54.

Railo ni wakala wa mchezaji Paul Pogba, Erling Haaland, Zlatan Ibrahimovic na Marco Verratti, Henrikh Mkhitaryan, Gianluigi Donnarumma lakini pia aliwahi kumsimamia mshambuliaji wa Everton, Moise Kean aliyopo kwa mkopo Juventus sambamba na mtukutu ‘super’ Mario Balotelli kipindi cha uhamisho wake pale Liverpool mwaka 2014.

Hivi karibuni wakala uyo aliripotiwa kuwepo nchini Ujerumani akipatiwa matibabu ya tatizo la upumuaji ambalo alihusiani na ugonjwa wa Corona kabla ya kuibuka kwa taarifa kupitia Luninga ya Italia ya Tg La7 kufariki Dunia siku ya Alhamisi.
Wakala huyo machachari na mwenye jina kubwa barani Ulaya hasa kuhusiana na sajili ngumu na tata za wachezaji wake amezaliwa mwaka 1967 nchini Italia.
Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button