Burudani

TANZIA: Rapper chipukizi aliyeshika namba moja Billboard auawa kwa kupigwa risasi

Rapper Jahseh Dwayne Onfroy ambaye anafahamika kwa jina la XXXTentacion amefariki dunia kwa kupigwa risasi mjini Florida, Marekani.

Kwa mujibu wa jeshi la polisi limesema kuwa XXXTentacion, 20, ameuawa kwenye maeneo ya Broward County mjini humo Jumatatu hii baada ya kuvamiwa akiwa kwenye gari lake akiwa ametoka kwenye duka la pikipiki.

Akiongea na shirika la habari la CNN, Afisa Habari kwa pilisi wa Sheriff, Keyla Concepción, amesema watu wawili waliovalia mavazi ya rangi ya giza walimvamia msanii huyo na kumuuwa hadharani.

Rapper huyo chipukizi amewahi kushika namba moja kwenye chati za billboard Hot 200 kupitia albamu yake ya ‘?’ March 16, 2018 ambapo ndani yake ina ngoma zinazohit kwa sasa kama ‘Sad!’ na ‘Changes’. Isikilize ngoma yake ya Sad hapa chini.

Related Articles

Back to top button