TECNO kutwaa tuzo ya simu pendwa baada ya kuishinda Samsung

Utafiti wa soko la teknlojia, uliofanywa na Kampuni ya utafiti ulimwenguni inayojishughulisha na bidhaa katika tasnia ya teknolojia ya vyombo vya habari na mawasiliano ya simu. Mwishoni mwa mwezi wa nne wametoa report ikionyesha kuwa kampuni ya simu TECNO imechukua nafasi ya kwanza kama simu bora Afrika kwa mwaka 2020 baada ya kuipindua kampuni ya simu Samsung na hii ni kufuatia uzalishaji wa simu za TECNO kuwa na viwango vya kuridhisha na kwa bei rafiki.

                                     :Rekord za shirika la usafirishaji wa simu janja Afrika 2020.

TECNO imefanikiwa kuwa kinara kufuatia anguko la asilimia 6.7% katika usafarishaji wa simu janja barani Afrika mnamo mwaka 2020. Uharibifu mkubwa ulifanyika katika nusu ya kwanza ya mwaka kwa sababu ya usumbu wa usambazaji uliosababisha na COVID-19, nakupelekea uhitaji kuwa mkubwa katika nusu ya pili.

Akizngumza juu ya mienendo ya soko, Mchambuzi Muandamizi Yang Wang alisema, kuangalia mwaka mzima soko la simu janja Afrika katika mikoa yake lilifanya vizuri lakini haikuweza kupigana na uharibu ulioletwa na COVID-19.

Robo ya pili ya mwaka 2020 ulikuwa mgumu zaidi baada ya uhitaji kuwa mkubwa lakini nchi nyingi zilikuwa zinapitia sheria ya kujifungia ‘lockdown’. Usafirishai wa simu janja wakati wa robo ya pili ulisababisha kushuka kwa asilimia 27%.

                                     :Rekord za shirika la usafirishaji wa simu janja Afrika 2020.

Wang aliongeza, vizuizi vilianza kushuka mwezi Julai. Mahitaji yalifuata vivyo hivyo na kuongezeka kwa shughuli za uendelezaji, hata wakati kesi za COVID-19 zilipopanda juu kuelekea msimu wa ununuzi Christmas. Robo ya 4 kwa mwaka 2020 ilitoa faida ya asilimia 1.5% kwa maeneo ya robo bora zaidi kwenye rekodi.

Kulingana na report, TECNO ilikuwa namba moja katika mwaka 2020 licha ya kuwa soko la simu liliyumba barani Afrika kutoka na janga la COVID-19 hali ilipoanza kuwa shwari TECNO ilifanya vizuri sokoni kutokana na uzalishaji wa simu bora kwa bei rafiki.

TECNO iko tayari kupata faida zaidi kwa 2021. Samsung imeona soko lake likishuka kutokana na mvurugiko wa usambazaji wa mapema mwanzoni mwa mwaka, TECNO imekuwa kwa kasi barani Afrika na kufikia hadi nchi 60 na zaidi barani Asia, Latini America na Middle East katika miaka ya hivi karibuni huku lengo lake kuu likizingatiwa kwa uendaji sambamba na teknolojia katika bidhaa mpya na kufikia vijana zaidi.

Mabadiliko makubwa yameonyeshwa na TECNO CAMON na TECNO Spark Series zilizozinduliwa mnamo mwaka 2020 na kuzingatia teknolojia katika mfumo wa camera.   

Related Articles

Back to top button