MahojianoPicha

TECNO Phantom 9 yapokelewa kwa shangwe na Watanzania

Ni takribani mwezi mmoja sasa umepita tangu, Kampuni pendwa hapa Tanzania ya simu za mkononi ya TECNO, Kuingiza sokoni simu yao mpya ya toleo la simu janja ya Phantom 9.

Gabo

Toleo ambalo limekuja na Kamera tatu za nyuma zenye Megapixel 16, 8 na 2 huku Kamera ya mbele ikiwa na Megapixel 32, Ambapo kwenye kampuni hiyo linakuwa toleo la kwanza kuwa na kamera 3. Je,  wadau wamelipokeaje toleo hili la simu za Phantom 9?

Tumefanya mahojiano na baadhi ya wateja walionunua toleo hilo la simu na kila mmoja ameeleza kitu kilichomvutia.

“Nimekuwa mtumiaji wa simu za Tecno toka miaka hiyo, Lakini hii phantom 9 jamaa wametisha sana hususani kwenye mambo ya picha picha yaani wameboresha sana,” amesema Ally Nassor mkazi wa Kigogo Dar es Salaam.

“Sijawahi kutumia TECNO katika maisha yangu, Ila hii Phantom 9 ina nyingi zilizonishawishi kununua. Inatunza Sana chaji. Mara ya kwanza niliiona kwa mke wangu, Nikaanza kuitumia baada ya kupoteza simu yangu ya awali. Kuanzia hapo simu hii ilinishawishi sana nikaamua na mimi ninunue ya kwangu, Tecno nawaelewa sana.” – amesema Mtumiaji mpya wa Phantom 9 aitwaye Charles Ngimbo.

“Hii simu nimeipenda zaidi kwenye Kamera na ukubwa wa ndani. Yaani hakuna kitu kilikuwa kinanikera kama napiga picha halafu naambiwa simu imejaa nifute vitu kwanza ndio nipige picha. Ila phantom 9 nimeikubali yaani GB 128 ziwezi kujaza hata nipige picha miaka mitatu.” – amesema Asha Ramadhan.

“Unajua mastaa wengi wanakariri heti Tecno sio simu nzuri. Mimi hii Phantom 9 ndio simu yangu bora kuliko simu yoyote kwa sasa duniani. Nawambia waache kukariri wanunue hii simu wajionee maajabu,”- amesema Muigizaji wa filamu, Gabo Zigamba.

“Tecno ninachowapendea wanatoa simu kali halafu bei iko poa. Yaani kwa sifa za Phantom 9 nilijua watauza bei kubwa kumbe ni rahisi tu. Mimi leo nimenunua simu mbili za Phantom 9 moja nitampa mke wangu anapenda sana kupiga picha,” amesema Peter Emmanuel Nkonto.

Simu za TECNO Phantom 9 zipo madukani na zinapatikana kwa bei ya kuanzia laki 6 hadi laki 6.5 .

Soma sifa nyingine za Tecno Phantom 9 HAPA.

Related Articles

Back to top button