TECNO Yagusa Hisia: Mchezo wa Hisani Wachochea Hamasa ya Kuboresha Viwanja vya Jamii Barani Afrika
Kama mdhamini rasmi wa Kombe la (AFCON) Afrika nchiniCôte d’Ivoire, kampuni ya teknolojia , TECNO iliandaa mechiya hisani iliyojaa nyota magwiji wa mpira wa miguu Africa sikuya pili ya sherehe ya ufunguzi. Mechi hiyo ilishirikisha KatibuMkuu wa CAF, Véron Mosengo-Omba, wachezaji maarufu wampira akiwemo Jay-Jay Okocha, El Hadji Diouf, AsamoahGyan, Dennis Oliech, na Erick Otieno, waliyoonyeshaushirikiano wao kwa michezo na maendeleo ya jamii.
Meneja Mkuu wa TECNO Akishikana Mkono na magwiji waSoka Afrika
Picha ya pamoja Timu ya CAF Pamoja na magwiji wa SokaAfrica
Kabla ya kuanza kwa mchezo wa kirafiki, TECNO ilitangazampango wa kufadhili matengenezo ya viwanja 100 vya mpiravya jamii zote Afrika ndani ya miaka mitano ijayo. Mpango huuunalenga kuhamasisha ushiriki wa vijana, kukuza maisha yenyeafya, na kuhakikisha upatikanaji wa viwanja bora vya michezokatika jamii zisizopewa kipaumbele. Meneja Mkuu wa TECNO, Jack Guo, alisema kwa hamasa, “Tumeanzisha safari ya kuzitiamwangaza ndoto zisizohesabika kwa kuboresha viwanja 100 kote Afrika,” akisisitiza nguvu ya kubadilisha ya mpango waTECNO. Taylan Tankpinou, mvulana wa miaka 10, aliongeza, “Asante kwa TECNO, tunajenga maeneo bora ya kuchezea nakukua!
Hotuba ya Mpango wa Kifadhili
Ili kuhamasisha zaidi, TECNO ilitangaza kwamba kwa kila golilililofungwa katika mchezo huo liligharimu, dola $10,000 ambazo zingechangiwa kwenye kampeni hiyo. Mchezoulimalizika na TECNO kuchangia dola $50,000 zaidi kwa mradihuo. Ahadi hii ilifanya kila goli kuwa shangwe si tu kwawachezaji bali pia kwa vizazi vijavyo ambavyo vitafaidika namiundombinu bora.