BurudaniHabari

Tekashi alazwa kwa kuumizwa mbavu na mgongo

Baada ya video kusambaa mitandaoni zikimuonyesha Rapa #6ix9ine akipigwa katika eneo la kufanyia mazoezi Gym na baadaye kukimbizwa Hospitalini.

Taarifa zinasema kuwa Tekashi amelazwa Hospitali Baada kuvamiwa na kupigwa na kundi La watu Akiwa Gym Huko Kusini Mwa Florida.

Wakili Wa #6ix9ine, Lance Lazzaro Ameiambia TMZ kuwa jamaa amejeruhiwa Kwenye Taya, Mgongo Pamoja Na Ubavu, taarifa yake ilieleza kuwa 6ix9ine alikuwa ndani ya Gym ya sauna wakati tukio Lote Hilo Linatokea La kuvamiwa Na watu hao, hata hivyo alijaribu kupambana nao lakini walikuwa wengi na hakuwa na ulinzi (Bodyguard) kwa wakati Huo”.

Wafanyakazi wa Gym walisikia zogo na kutoa taarifa kwa Meneja lakini pia Jeshi La Polisi Na Ems Waliitwa Na Eneo La Tukio Kisha Kumkimbiza 6ix9ine Hospitali na Ambulance

Wengi wanaamini kuwa huenda ni lile kunndi la washikaji zake wa “Nine Trey Gangsta Bloods” aliowa-Snitch waende Jela mwaka 2020 ambapo yeye aliachiowa huru lakini bado Haijajulikana kama uvamizi Huo Unahusiana Na Masuala Yake Ya U-Snitch.

Mbali na hilo wengine wanaamini huenda jamaa anatengeneza Attention (kiki) kwa kuwa alikaa kimya sana huenda kuna jambo lipo njiani aidha na wimbo au project yoyote ile.

Wewe unaamini vipi ni kweli au kiki??

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents